COSTECH yatumia Sh bilioni 4.2 kuwezesha wabunifu

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetumia zaidi ya Sh.

Bilioni 4.2 kwa wabinifu 178 ili kuendeleza ubunifu uliofanywa na watafiti wa kitanzania katika kuhakikisha kuwa unawanufaisha watanzania kwa kubadilisha maisha yao.

Aidha COSTECH pia imefanikiwa kuwatambua wabunifu 2647 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.

Akizungumzia na habariLEO, Mwakilishi wa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MTUSATE) Dickson Mjarifu amesema wabunifu 283 wamepatiwa msaada wa kitaalamu kutoka katika taasisi mbalimbali za kiserikali ili kuendeleza bunifu zao kwa manufaa ya nchi na watanzania wote.

“kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 COSTECH tumewatambua wabunifu 2647 katika ya hao 283 wamepatiwa msaada wa kitaalamu na 178 wamepatiwa fedha ili kuendeleza bunifu zao na ”amesema Mjarifu.

Mjarifu amesema kuwa baadhi ya wabunifu waliofaidika na COSTECH ni pamoja na mtanzania aliyebuni Majipesa ambapo mtu anaweza kuweka hela kujipatia maji kulingana na kiwango cha fedha alizoweka.

“MAXCOM Afrika na nyingine nyingi ikiwemo mita za maji ambazo unalipia kabla ya matumizi.

Habari Zifananazo

Back to top button