CUF, CHAUMMA kuzindua kampeni leo

DAR ES SALAAM: Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) wanatarajia kuzindua kampeni za Uchaguzi Mkuu wa wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumapili Agosti 31 2025.

Mgombea urais wa CHAUMMA, Salum Mwalimu, na mgombea mwenza, Devotha Minja, watakuwa katika viwanja vya Kinondoni Biafra jijini Dar es Salaam badala ya Temeke kama taarifa za awali zilivyoeleza.

Chama cha Wananchi (CUF) kitazindua kampeni zake leo Uwanja wa Furahisha, uliopo Wilaya ya Ilemela, Mwanza, ambapo mgombea urais wa chama hicho, Samandito Gombo atanadi sera zake kwa wananchi wa mkoa huo.

CUF imesema sababu za kuamua kuzindua kampeni zake jijini Mwanza ni kwa sababu mkoa huo ni wa kimkakati, kisiasa, lakini pia ni nyumbani kwa mgombea wake wa urais na wanatarajia kuungwa mkono.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button