Dani Alves afikishwa mahakamani kwa ubakaji

MLINZI wa kulia aliyewahi kucheza Barcelona, Dani Alves amefikishwa mahakamani nchini Uhispania akituhumiwa kumbaka mwanamke akiwa katika kumbi moja ya starehe usiku.

Dani ,40, amekuwa gerezani bila dhamana kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu kisa hicho kinachodaiwa kufanyika Desemba 2022.

Imelezwa kuwa beki huyo wa Brazil huenda akafungwa jela miaka 12 iwapo atapatikana na hatia.

Dani amekanusha kukutana na mshtaki wake, lakini baadaye alisema walifanya ngono kwa makubaliano. Kesi yake itakamilika Jumatano.

Zaidi ya watu 30 akiwemo Dani Alves na mkewe waliyeachana nao wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.
Mahakama ya Barcelona siku ya Jumatatu ilikataa ombi lake la kuahirisha kesi hiyo ili apewe muda zaidi wa kujiandaa.

Habari Zifananazo

Back to top button