Dar City yatetea ubingwa mara ya tatu mfululizo

DAR ES SALAAM: Dar City imetetea ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Stein Warriors pointi 66-50 katika mchezo wa mwisho wa fainali uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa IST, Masaki.

Ushindi huo umeifanya Dar City kufunga mfululizo wa fainali kwa ushindi wa michezo mitatu mfululizo dhidi ya Stein Warriors na kuendelea kutawala mashindano hayo kwa mara nyingine.

Dar City imeonesha ubora wake katika michezo hiyo ya fainali na kufanikiwa kuhifadhi taji hilo, huku Stein Warriors ikishindwa kuzuia wapinzani wao kufikia lengo la kutetea ubingwa.

Kwa upande wa wanawake, Reel imetwaa taji hilo baada ya kuichapa Tausi Royal kwa pointi 81-54.

Reel inasimamiwa na mwanamuziki Emanuel Mkono ‘Nahreel’ ikiwa ni mara ya kwanza inachukua taji hilo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button