Dar es Salaam sasa ni kijani

KAMPUNI ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kushirikiana na Kampuni ya African Carbon Agency imezindua zoezi la upandaji miti katika vituo vya mabasi ya mwendokasi kutoka Morroco kuelekea Magomeni lengo kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kijani yenye hewa safi.

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi hilo leo Januari 14, jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa DART, Dk Athuman Kihamia lengo ni kupanda miti milioni moja kwenye korido zote za mwendokasi.

Advertisement

“Hii ni sehemu ya kwanza tutakuwa na awamu sita zitakazochukuwa mabasi takribani 3,000 sasa njia ni nyingi zote tunatarajia ziwe na miti,” amesema Kihamia.

Aidha, amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuwa mabalozi wazuri wa kuhakikisha miti hiyo inatuzwa ili ilete hewa safi.

Mwakilishi wa African Carbon Agency, Rahim Kangezi amesema hatua hiyo ni mwanzo kwani lengo lao kubwa ni kuifanya Dar es Salaam kuwa yenye hewa safi inayovutia.

“Tunachojaribu ni kuiunga mkono serikali kuhakikisha hili jambo tunalifanya kwa ukubwa,” amesema Kangezi.