DC Arusha ataka uadilifu kamati ya michezo wilaya

ARUSHA: MKUU wa Wilaya Arusha Mjini, Joseph Modest Mkude ameisisitiza kamati ya michezo wilaya kufanya kazi kwa uadilifu na bidii ili kuhakikisha michezo inakuwa chombo cha kuibua vipaji, kumarisha afya, ajira na kuhamasisha utalii.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kamati ya Michezo Wilaya iliyoteuliwa hivi karibuni, mkuu huyo amesema serikali ya wilaya ipo pamoja na wajumbe hao kuhakikisha wanapata ushirikiano na nyenzo za utekelezaji.

“Nawasisitiza wajumbe wa kamati kufanya kazi kwa uadilifu, mshikamano na bidii na tunaziomba sekta binafsi na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi hizi kwani michezo ni jukumu la jamii nzima,”amesema Mkude.

Amefafanua kuwa uzinduzi wa kamati hiyo ni hatua ya kimkakati inayolenga kuratibu na kusimamia shughuli zote za Michezo Wilaya ili kuwa na muundo rasmi na endelevu ,kukuza,kuibua vipaji vya michezo kuanzia ngazi za chini yaani shuleni,mtaa,kata hadi taifa.

Aidha, Mkude ameeleza kuwa Arusha inapokaribia kuwa sehemu ya maandalizi ya mashindano makubwa ya AFCON ni lazima kuanza kujiandaa na kujifunza mapema lengo nikuifanya Arusha kuwa kivutio kukuu cha michezo pia.

“Tuna kila sababu ya kufanikisha hili kutokana na historia yetu, mazingira na nguvu kazi hivyo pia ni matarajio makubwa kuona Arusha ikipata timu ya ligi kuu kama alivyobainisha mkuu wetu wa Mkoa Amos Makalla hivyo nasi tuwe mstari wa mbele kuhakikisha hilo na linawezekana tukihamasishana, kushirikiana na kuziunga mkono timu zetu,” ameongeza Mkude.

Pia amesisitiza kuendelea kuhamasisha uwekezaji kwenye michezo kwa kujenga miundombinu bora, kuratibu na kutoa fursa mbalimbali za mafunzo ili kuwa na wataalamu wa kutosha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button