DC Ileje ahamasisha ushiriki wa uchaguzi

SONGWE: Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi, ameendelea kutoa hamasa kwa wananchi wa wilaya kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Siku ya leo, DC Mgomi ametembelea vikundi vya maofisa usafirishaji ‘bodaboda’ wa vijiji vya Itumba, Isongole na Shinji, ambapo amewahimiza vijana hao kuwa mabalozi wa amani na kuhubiri utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi.

Katika hamasa hiyo, Mgomi aliwaasa vijana hao kukemea na kutokuruhusu viashiria vyovyote vinavyoweza kuvunja amani, akisisitiza kuwa jukumu la kulinda utulivu ni la kila mwananchi.
Aidha, DC Mgomi amewahakikishia vijana hao kuwa Wilaya ya Ileje itaendelea kuwa salama kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali na maendeleo.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na vijana katika kujenDC Ileje ahamasisha ushiriki wa uchaguziga mazingira rafiki ya ajira na biashara, ili kuwawezesha kuongeza kipato chao na kuchangia katika kukuza uchumi.



