DC Kahama ataka wakulima wa tumbaku kupewa kipaumbele

SHINYANGA: MKUU wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Mboni Mhita ameziomba taasisi za fedha kuendelea kuwajali wakulima wa zao la tumbaku kwani ekari 500 za zao hilo zilihalibiwa na mvua ya mawe iliyonyesha hivi karibuni.
Mhita amesema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilayani humo (KACU) ambapo ameeleza baada ya mvua hiyo kunyesha wataalamu walifanya utafiti nakubaini kilo 190,000 za tumbaku zimepotea.
“Rais Samia Suluhu kupitia serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha miaka minne ameweza kutoa fedha nyingi katika sekta ya kilimo nakuanzisha mradi wa jenga kesho yako (BBT) kwa kuhakikisha maofisa kilimo kwenye kila kata,”amesema Mhita.

Meneja Mahusiano wa Kitengo cha zao la tumbaku kutoka Benki ya NMB, Jacob Laurian amesema hapa nchini zaidi ya wakulima 2000 wamenufaika na malipo ya fidia kwa zao la tumbaku kwa nchi nzima sawa na Sh bilioni 1.2. kwa mwaka 2023/2024.
Laurian amesema mwaka 2023/2024 benki hiyo ilitoa mkopo kwa wakulima Dola milioni 90 na mwaka 2024/2025 walitoa Dola milioni 108 na fedha hizo ni kwa ajili ya zao la tumbaku pekee.
Naye Meneja wa Mahusiano na Kitengo cha Biashara na zao la tumbaku Kanda ya Magharibi, Alpha Manota amesema tayari wamekopesha vyama 214 vya msingi na mwaka huu wamekopesha vyama 23 vya msingi.

“kwanza inapofika mwezi Septemba na Oktoba tunatoa elimu kwa wakulima na tunakopesha fedha hizo kwaajili ya kufanya maadalizi ya kununua kuni na miti, kujenga bani na kununua pembejeo kwa ajili ya zao la tumbaku,”amesema Manota.
Mwenyekiti wa KACU Emanuel Nyambi akiongoza mkutano huo pamoja na wajumbe wa bodi wametaja vyama vilivyozalisha vizuri zao la tumbaku na Pamba kwa msimu uliopita huku Mkuu wa Wilaya akitoa zawadi ya vyeti vya pongezi.
Vyama vilivyozalisha vizuri zao la tumbaku ni Kipalapala, Ngokolo, Nonwe na zao la pamba ni Muungano, Balimi na Kazana na vyama vyenye uongozi bora ni Uyogo na Kipalapala na viluvyofanya uwekezaji ni Mkombozi, Uyogo na Kipalapala .




Ultimately, I was able to recover $48,500 of my initial deposit, a result I had almost abandoned hope of achieving. My experience served as a valuable lesson. The crypto gaming sector is fraught with hidden dangers, and not every platform is as trustworthy as it presents itself to be. Thorough research is essential, and seeking support from DUNE NECTAR WEB EXPERT is advisable if you encounter Cryptocurrency Fraud.
– Te/eGram – @dunenectarwebexpert