DC Mwenda: Asante sana Rais Samia

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Yusufu Mwenda amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani hiyo.

Katika taarifa yake ya kuukaribisha mwaka mpya 2025, DC Mwenda amemshukuru pia Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dk Mwigulu Nchemba kwa kuendelea kutekeleza ilani kwa vitendo kwa kuhakikisha wananchi wa Iramba wanapata huduma bora za kijamii.

Ametaja huduma hizo kuwa ni afya, elimu, maji na kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo isiyokuwa na riba mampato ya ndani ya halmashauri.

Advertisement

“Niwashukuru sana watumishi wa ofisi ya mkuu wa wilaya wakiwemo makatibu tawala Warda Abdallah Obathany, Stella Msofe, Bupe Mwakibete na watumishi toka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Iramba kwa ushirikiano walionipatika katika kuhakikisha tunawatumikia wananchi wa Wilaya ya Iramba ,”

“Tuendelee kuwaombea wale wote walio hospitali wakiendelea na matibabu, Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa afya njema waweze kupona na kurudi kwenye majukumu yao ya awali,” amesema DC Mwenda.