DC Mwenda ashiriki upandaji miti hospitali ya Mandewa

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda ameshiriki zoezi la kupanda miti katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.

Zoezi hilo limefanyika leo Desemba 9, 2024 kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singid, Ester Chaula.

Zoezi Hilo la upandaji miti limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania bara ambayo huadhimishwa Desemba 9.

Jumla ya miti 501 imepandwa katika eneo la Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.

Habari Zifananazo

Back to top button