DC Mwenda ataka kipaumbele cha lishe Iramba

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kulipa kipaumbele swala la lishe katika jamii.

Mwenda ameyasema hayo Novemba 1, 2024, katika viwanja vya Halmashauri wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe.

Advertisement

DC Mwenda amesisitiza umuhimu wa kuwa na bustani ya mbogamboga katika shule zote za Msingi na Sekondari zilizopo wilayani Iramba, ili kuwajengea wanafunzi utamaduni wa lishe bora kwa vitendo.

Aliongeza kuwa shughuli hizi zinapaswa kuanzia uzalishaji, uandaaji, na matumizi ya mboga mboga kwa wingi, hivyo kuitengeneza jamii inayojali afya bora kupitia lishe bora.

Aidha, alishauri kuwepo kwa kitalu nyumba (greenhouse) katika moja ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, kitakachosaidia katika upatikanaji wa lishe bora kwa wanafunzi wote wakati wote wa mwaka.

Mwenda pia alisisitiza umuhimu wa kuingiza ajenda ya lishe katika vikao vya kata ili kufuatilia kwa ukaribu mafanikio na changamoto, kwa lengo la kuikomboa jamii kutoka kwenye madhara ya lishe duni, kama vile magonjwa yasiyoambukizwa kama shinikizo la damu na kisukari.


Ofisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Joyce Maganga amesema kuwa ,halmashauri hiyo inatoa huduma za afya kupitia vituo 47,ikiwemo ushauri wa masuala ya lishe katika jamii.

Maganga amesisitiza Wazazi kuhakikisha watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanapata mlo wenye makundi sita ya vyakula ili kuwalinda na udumavu wa mwili na akili, ambao huathiri uelewa wao darasani