MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amewaalika wananchi wote, wakulima, wafugaji, wavuvi, watumishi wa umma na mashirika na asasi binafsi kuhudhuria kongamano la ufunguzi wa msimu wa kilimo kwa mwaka 2024/2025 litakalofanyika kimkoa wilayani Iramba.
Kongamano hilo litafanyika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya (Mabatini) kuanzia Novemba 1 -2, 2024.
Huduma mbalimbali na ushauri vitatolewa kwenye kongamano hilo ikiwa ni pamoja na upimaji wa afya ya udongo, uuzaji wa mbegu na mbolea za ruzuku ,viwatilifu na chanjo kwa bei nafuu, usajili wa wakulima kwenye mfumo wa pembejeo na ruzuku ili kupata namba ya mkulima.
Aidha Burudani mbalimbali zitakuwepo wakati wa Kongamano na mada mbalimbali zitatolewa kwenye Kongamano kama vile ;
-Ruzuku ya mbolea na mbegu za mahindi
-Kilimo cha mbaazi
-Mfumo wa stakabadhi ghalani
-Mifugo inalipa
– Fursa za uwekezaji na utalii katika Ziwa Kitangiri.
Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo anatarajiwa kuwa Halima Omary Dendego Mkuu wa Mkoa wa Singida