DC Mwenda ataka amani sikukuu chrismas Iramba

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka Wananchi wa Wilaya ya Iramba kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2025 kwa amani na utulivu.

“Tunaposherehekea sikukuu hii ya Christmas, nawatakia heri Wananchi wa Wilaya ya Iramba.
Ikawe siku ya mapumziko yaliyo mema yenye furaha, upendo na mshikamano,” amesema Mwenda.

Akitoa salamu za Sikukuu ya Krismasi Jumanne Disemba 2024 Mjini Kiomboi, DC Mwenda amewataka wananchi kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa amani na utulivu bila kusababisha vurugu.

Advertisement

“Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kukabiliana na mtu yeyote atakayesababisha uvunjifu wa amani, tutamchukulua hatua za kisheria,” alisema DC Mwenda

Aidha Mwenda amewataka watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu kuhakikisha wanazingatia Sheria za usalama barabarani.

“Tuhakikishe tunawalinda Watoto wetu kwa kuwakumbusha kuchukua tahadhari wanapokuwa barabarani pia kuepuka msongamano usiokuwa wa lazima kwenye mikusanyiko “