Diamond Platnumz apata ‘shavu’ ubalozi vitenge vya wax

WATENGENEZAJI na wasambazaji wa kimataifa wavitambaa na vitenge vya wax, HOLLANTEX wamemtangaza msanii wa muziki wa Bongo flava Diamond Platinumz kuwa balozi mpya wa chapa ya bidhaa zao nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na HOLLANTEX, makubaliano yamefikiwa na msanii huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka mtindo wake wa kucheza jukwani akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni yenye rangi tofauti hali ambazo zinawavutia watazamaji wake sio tu kucheza muziki wake bali pia kupenda mavazi yake ya nguo za vitenge zenye rangi bora za kitamanduni na za kuvutia.

Katika makubaliano ya ubalozi wake mpya, Diamond Platnumz atatumia kazi zake za kisanii kunadi rangi bora za bidhaa zitolewazo na kampuni ya Hollantex, zenye muundo na ubora wa hali ya juu ambazo zinalenga kutatua uhaba wa muda mrefu wa mavazi ya kitamaduni ya ubora wa vitenge vya wax katika soko la tanzania na barani Afrika kwa Ujumla.

“Kwa kupitia ubalozi wa Diamond katika bidhaa hizi ni wakati muafaka sasa kwamba watu nchini Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki sasa wanaweza kujua uwepo wa vitenge na vitambaa bora vya Wax sokoni vya chaguo lao,” taarifa hiyo inamnukuu mwanzilishi wake, Thomas Fournier akisema.

Hollantex huzalisha na kusambaza vitambaa na vitenge vya wax vyenye rangi maridadi zaidi vilivyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu sana. Kauli mbia ya bidhaa za kampuni hii ni “Rangi yako, maisha yako.”

Hollantex pia imejikita zaidi katika ubunifu, utengenezaji, na uuzaji wa vitambaa na vitenge bora vya wax vyenye kubeba historia ya Kiafrika na mitindo ya Magharibi na daima ni ubunifu katika suala la utaalamu ya rangi ili nzuri.

“kuvutia zaidi wateja wake na kuhakikisha juu ya uwepo wa bidhaa za Hollantex nchini Tanzania ambao utatengeneza fursa za Biashara kupitia soko la mavazi kwa watanzania ili kuinua uchumi wa nchi,” taarifa ya kampuni inasema.

Kampuni hiyo ilitangaza kwamba hatua hiyo ilifikiwa baada ya mtaalamu wa sayansi ya rangi za mavazi Thomas Fournier, kutembelea sehemu mbalimbali za Afrika na kukutana na uzuri wa bidhaa za vitambaa vya wax ambazo huchanganywa kwa uangalifunwa rangi na michoro ili kuonyesha tamaduni nzuri zaidi kwa wakazi wa bara hili
Fournier anasema kuwa katika ziara yake hiyo. aligundua kwamba uwepo vitambaa na vitenge vya Wax bora masokoni havikuwa vya kutosha kukata kiu ya wateja katika masoko mbalimbali.

“Kwa hiyo ubalozi huu wa Diamond unalenga kuwajulisha wafuasi wa mziki wake kuwa sasa bidhaa hizo ziko sokoni ni wakati Kiafrika kukutana na rangi hizo kuvutia na hivyo basi, kila mtu anaweza kuvaa kitambaa chake bora cha kitenge cha wax, afurahie kila siku ya maisha yake ya kupendeza.

Mbali na kuwa na uwepo na kufanya mauzo nchini Tanzania, kampuni hiyo pia inauza bidhaa katika nchi nyingine za kiafrika kama vila, Ivory Costa, Nigeria, Ghana, Togo, Benin, Niger, Mali, Guinée na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi nyingine nyingi barani Afrika.

Diamond anaungana na wasanii wengine maarufu wa Kiafrika ambao pia ni mabalozi wa bidha za Hollantex; kama vile Yemi Alade, Fally Ipupa, Sidiki Diabate; Toke Makinwa na Nancy Isime ambao wamekuwa sehemu ya timu ya Hollandex kwa miezi kadhaa katika kunadi vitenge hivyo yenye rangi murua vya ubora wa daraja la juu katika ubora.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button