DIB yatoa elimu ya Amana

BODI ya Bima ya Amana (DIB) iliyopo ndani ya jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) inatoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya amana na uhakika  wa kupata fedha zao pale benki inapofilisika.

Bodi hiyo inashiriki Maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya sabasaba  ambapo elimu inayotoa ni namna ambavyo bodi hiyo inalipa fidia wenye amana zilizokingwa endapo benki au taasisi ya fedha imeanguka.

Akizungumza na HabariLeo, Joyce Shala Afisa Mwandamizi kutoka bodi hiyo anasema  bodi hiyo ina majukumu ya  kukusanya michango kwa mabenki na taaissi za fedha zilizopewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania, jukumu la pili ni kuwekeza michango katika dhamana ya serikali kwa muda mrefu na dhamana ya muda mfupi.

Advertisement

Amesema lengo kuu la kufanya uwekezaji huo ni kutunza mfuko, kulipa fidia kwa wananchi pale ambapo benki au taasisi za fedha zitaanguka na kufungwa na benki kuu na jukumu lingine ni kufanya ufilisi

Amesema, DIB inalipa fidia wenye amana zilizokingwa endapo benki au taasisi ya fedha imeanguka.

“Kwa sasa kuanzia Februali Mosi, 2023, amana zinakingwa hadi kufikia ukomo wa shilingi milioni 7.5  sawa na kiasi cha dola za Marekani 3,250.00 kwa kila mwenye amana katika benki.”Amesema na kuongeza

“Kiwango cha juu cha sasa cha shilingi 7,500,000 kinakinga asilimia 97.1 ya jumla ya idadi ya akaunti za amana. Ulipaji fidia kikamilifu kwa amana zilizokingwa unakuza imani ya umma katika mfumo wa kibenki na hivyo kuchangia katika utulivu wa sekta ya fedha nchini.”Amesema

Amesema, ulipaji fidia kwa amana za benki  zilizofungwa unaendeshwa na DIB kwa kushirikiana na BOT kupitia ofisi kuu za benki zilizofungwa.

 

2 comments

Comments are closed.