Dk Ashatu asisitiza manunuzi ya bidhaa za ndani

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Dk Ashatu Kijaji amewataka Watanzania kuacha kununua bidhaa zinazotoka nje ya nchi Ilihali zinazalishwa nchini na Kwa viwango vyenye ubora unaokidhi matakwa.

Amesema hayo leo Dar es Salaam baada ya kutembelea Viwanda vya Motisun (IMMI) vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo bati,nondo,plastiki,juisi na hata rangi.

Kuhusu bidhaa za ndani amesema vipo viwanda nchini vinavyozalisha bidhaa zenye ubora unaostahiki na kwamba Watanzania waache kukimbilia nje ya nchi,badala yake wanunue zinazozalishwa nchini.

“Tanzania ina viwanda vinavyotengeneza bidhaa nzuri zisizo na mashaka, bidhaa hizo zina viwango vyote vinavyotakiwa na Taasisi za ukaguzi,” amesema Dk Kijaji na kuongeza kuwa wakati Taifa likielekea kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2024 ni vyema kuona namna ya kumlinda viwanda Kwa manufaa ya Watanzania.

Aidha amewataka wenye viwanda kuwa wavumilvu kwenye changamoto ya umeme na kwba ni Kwa kipindi kifupi na ifikapo Februari kama ilivyoahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan suala litafikia mwisho.

Amesema Tanzania inaonuwezo wa kuzalisha bidhaa inayokidhi viwango vya juu kabisa ambapo ni wakati Sasa wa kuieleza Dunia juu ya bidhaa hizo ambazo zinakidhi matakwa ya soko.

Wakati hukohuko,Dk Kijaji almetumia muda huo kuhamasisha wenye viwanda hao kujipanga kupeleka bidhaa zao katika masoko mengi nje ya nchi ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Jumuiya ya Maendeleo Kusni mwa Afrika (SADC)na hata soko huru la Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MMI,Ratisy Kamamla amesema viwanda hivyo vinakabiliwa na changamoto ya kucheleweahewa maligajfi kutoka nje ya nchi haswa kupitia bandarini na kuomba suala hilo kufanyiwa kazi kwakuwa linarudisha nyuma uzalishaji.

Kadhalika amesema ipo changamoto ya umeme ambayo Kwa kipindi cha Oktoba Hadi Desemba mwaka jana wamekuwa wakikumbana na hasara Kwa kutofanya Kazi za uzalishaji.

Habari Zifananazo

Back to top button