Dk Kikwete aishauri CCM namna ya kuondoa uchimbi

“Simuoni Mwana CCM 2025 atakayechukua fomu kukupinga. Si mila yetu lakini ni seme ukweli, Hapa Tanzania kunamwanasiasa maarufu kumshinda Rais Samia? Usisumbuliwe na maneno hayo. Ni waombe ndugu zangu acheni uongo.

Ukiangalia huko mitandaoni kuna maneno mengi ya uongo, ni upuuzi tu. tuache hii tabia ndiyo inakigawa Chama chetu. Mnawafanya viongozi wetu wapate stress (jakamoyo) tu. Mkiwasikia watu wanasema maneno waiteni kwenye maadili na kama hana maelezo aambiwe aache uongo.

Hii ndio njia pekee itakayo ondoa uchimbi. Chama chetu ni kikubwa sana hakistahili kuvumilia upuuzi kama huo. Mkiuvumilia Chama hiki kitavurugika kwa maslahi ya wapuuzi. Naomba muwe wakali… Rais wa zamani, Dk Jakaya Kikwete akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari Zifananazo

Back to top button