Dk. Migiro: Tumewasha moto

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Asha-Rose Migiro amesema chama hicho kimewasha moto wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Dk Migiro alisema moto uliowashwa katika uzinduzi wa kampeni za CCM Dar es Salaam jana utasambaa katika mikoa yote. Alisema hayo kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers-Kawe wakati chama hicho kikizindua kampeni hizo kuomba kura kwa wananchi.

Dk Migiro alisema Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan aliwasihi na kuwaelekeza viongozi wa chama hicho wajipange kwa ajili ya kampeni na kuwataka uchaguzi uendeshwe kwa haki, amani na staha na kuwa umati huo uliojitokeza unaashiria wanawasha moto. “Leo (jana) tunawasha moto na baadaye moto huu utaenda mikoani,” alisema.

Alisema CCM imefanya maandalizi ya kutosha na kusema chama kitafanya kampeni za kistaarabu na kusisitiza kuwa wamedhamiria, wanamaanisha na wanakwenda kusaka dola na kuwa wako tayari kushirikiana na wengine. SOMA: Migiro: CCM itashinda kwa kishindo

Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Dk Emmanuel Nchimbi alisema yuko tayari kwa kazi. “Niko timamu kutekeleza maelekezo yako (mgombea urais kupitia CCM) na ya chama chetu ya kutafuta ushindi na baadaye kufanya kazi kwa juhudi kutekeleza Ilani ya CCM,” alisema Dk Nchimbi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button