Dk Mpango ataka umakini uvunaji madini

DODOMA: MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango ameitaka Wizara ya Madini kusimamia vyema uvunaji wa madini ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika nayo.

Dk Mpango amesema hayo leo Agosti 22, akiwa katika kata ya Mpwayungu Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma wakati akihitimisha ziara ya siku nne mkoani humo.

“Simamieni Kuna fursa nyingi upande wa Madini ujenzi hata kutengeneza mbolea, Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini haya mkakati kwa uwingi na aina tofauti tofauti,lazima rasilimali hii ikatafsirike katika maendeleo ya wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla,” amesema Dk Mpango.

SOMA: Mtambo wa kisasa uchimbaji madini wazinduliwa

Kiongozi huyo ameiagiza Wizara ya Madini kuhakikisha inaweka mpango mzuri wa usimamizi wa rasilimali hiyo kwa manufaa ya Taifa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Akiwasilisha salamu za wizara, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amemuahidi Dk Mpango kuyafanyia kazi maelekezo yote na kwa sasa Wizara inakamilisha andiko la mkakati wa usimamizi na uvunaji wa madini hayo ili yalete faida kwa nchi kwa kuchochea uchumi na kuendeleza sekta ya madini.

Mavunde alitumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Ofisa Madini Wakazi(RMOs) kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maeneo yenye uchimbaji wa madini mkakati ili manufaa yake yaonekane kwa taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button