Madini ya vito yavutia fursa ya uwekezaji

SPINEL ni mojawapo ya madini ya vito yenye thamani kubwa duniani, inayojipatia umaarufu mkubwa kimataifa kutokana na ubora wake, rangi adimu na uimara wa hali ya juu. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizojaa rasilimali hii adimu, hasa katika Mahenge, Kijiji cha Epanko, Wilaya ya Ulanga, mkoa wa Morogoro, eneo linalojulikana kwa kutoa spinel bora zaidi duniani.

Spinel ni jiwe lenye rangi mbalimbali ikiwemo nyekundu, pinki, zambarau, bluu na machungwa, lenye uwazi wa hali ya juu, rangi kali na uimara mkubwa unaofanya kudumu kwa muda mrefu; nyingi hupatikana bila matibabu ya joto, jambo linaloongeza thamani yake sokoni.

Spinel ya Mahenge, inayojulikana kwa rangi yake ya pinki na nyekundu yenye mwanga wa kipekee, imekuwa ikitajwa mara kwa mara katika maonesho makubwa ya kimataifa ya vito kama Tucson Gem Show (Marekani), Hong Kong Jewellery Fair na Bangkok Jewellery Fair, kuongeza hadhi ya Tanzania katika soko la madini ya vito duniani.

Uchimbaji wake unaendeshwa na kampuni za Kitanzania zikiwemo Ruby International Limited na Franone Mining, ambazo zinatoa mfano mzuri wa uwekezaji wa ndani katika rasilimali za taifa kwa uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria. Msimamizi wa Ruby International, Mhandisi Penina Mtego, amesema spinel ya Mahenge ni rasilimali adimu yenye ubora wa kipekee na kwamba kipaumbele ni ajira, maendeleo ya jamii na kulinda mazingira.

Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa, amesema madini ya vito kama spinel ya Mahenge ni utajiri mkubwa wa taifa na kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa ili rasilimali hizi zinawanufaisha wananchi, kuongeza mapato ya serikali na maendeleo ya nchi.

Uwepo wa migodi ya spinel umechochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa Mahenge, ikiwapa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, huku kampuni pia zikichangia ujenzi wa shule, zahanati, barabara na miradi ya maendeleo ya jamii. SOMA: WGC kuisaidia Tanzania kuongeza thamani ya madini

Uwepo wa madini ya spinel umechochea utalii wa madini, kuleta fursa katika malazi, usafiri, uuzaji wa vito na kukuza utamaduni wa wenyeji, huku spinel ya Mahenge ikionyesha jinsi rasilimali asili zinavyoweza kuleta maendeleo endapo zitasimamiwa kwa uwazi, uzalendo na uwajibikaji.

Kwa sasa, spinel inahitaji uwekezaji zaidi katika utafiti, uchimbaji, biashara na kuongeza thamani, huku ikizingatiwa kwamba Tanzania ina aina 25 tu zinazochimbwa kati ya zaidi ya 100 za madini ya vito, na Sheria inaruhusu wageni kushiriki kupitia mitaji na teknolojia.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button