Dk Mpango awapa mbinu vijana ufundi stadi

TANGA: Makamu wa Rais Dk Philip Mpango,amewataka vijana wanaosoma katika vyuo vya ufundi stadi kutumia ujuzi walioupata kutengeneza fursa ya ajira ambazo zitaweza  kuwanufaisha wao ,wazazi/walezi pamoja na jamii inayowazunguka.

Dk Mpango, ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika Chuo cha ufundi stadi kilichopo katika Kata ya Kasera Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Amesema uwepo wa vyuo hivyo utumike katika kuzalisha na kutengeneza fursa za ajira sambamba na wataalamu ambao wataweza kusaidia kuiletea nchi maendeleo.

Advertisement

Hivyo ili kuwaongezea umahiri vijana wanaopatiwa mafunzo na vyuo hivyo Makamu wa Rais amezitaka sekta binafsi nchini kutoa nafasi za mafunzo ya vitendo kwa vijana hao kwenye maeneo yao ili waweze kuwa mahiri kwenye fani walizozisomea.

Chuo cha veta Mkinga ujenzi wake umegharimu takribani Sh bilioni mbili na kinauwezo wa kudahili wanafunzi zaidi ya 240 kwenye fani mbalimbali.