Dk Mpango mgeni rasmi mkutano wadau wa siasa Arusha

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa kisiasa ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) utakaofanyika kuanzia Mei 8 hadi 10 mwaka huu jijini Arusha.
Hayo yamesemwa leo na Boniface Mwabukusi, Rais wa TLS alipozungumza na vyombo vya habari.
“Mkutano huo unalenga kuunganisha vyama vyote vya siasa nchini, na lengo lake ni kujadili namna nchi itakavyofanya uchaguzi kwa amani, bila vurugu,” alisema Mwabukusi.
Mwabukusi pia ameonya kuhusu mivutano ya kisiasa inayosababishwa na maneno yanayolenga kuchochea migogoro, ambayo inaweza kuleta vurugu na madhara kwa raia.
Aidha, Mwabukusi ameshauri umuhimu wa kufanya vyama vya siasa kufanya marekebisho madogo kwa wakati ili Watanzania waweze kuingia kwenye uchaguzi wakiwa na uhakika na amani.



