Dk Mwinyi afanya uteuzi wa viongozi

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi ameteua viongozi mbalimbali
Amemteua Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amemteua Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Pia amemteua Sadifa Juma Khamis kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
Amemteua, Othman Ali Maulid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja. Kabla ya uteuzi huo, Maulid alikuwa Mstaafu wa Utumishi wa Umma.
Amemteua, Galos Nyimbo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja. Nyimbo ni Mwanajeshi Mstaafu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka ofisi ya Baraza la Mapinduzi, wateule wote wataapishwa Septemba 20, 2023 saa 3:00 asubuhi, Ikulu, Zanzibar.