Dk Mwinyi amteua Sharrif Ali Sharrif

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amemteua Sharrif Ali Sharrif kuwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Taarifa kutoka Ofisi ya Baraza la Mapinduzi imeeleza Sharrif ataapishwa Februari 22, 2024, Saa 8:00 mchana katika ukumbi wa Baraza la Mapinduzi Ikulu-Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo Shariff alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji wa Zanzibar ZIPA

Advertisement