Tumaini jipya ujenzi shule ya kimataifa GEMS Zanzibar ukianza

Unguja. Ujenzi wa Shule ya Kimataifa ya GEMS Zanzibar katika eneo la mradi wa Infinity Hills unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Ujenzi huo ni hatua kubwa katika kupanua fursa za elimu visiwani humo kupitia shule iliyobuniwa maalum kuhudumia hadi wanafunzi 1,500.

Uwezo wa shule hiyo umeongezwa kutoka lengo la awali la wanafunzi 1,100 baada ya tathmini kuonyesha ongezeko la mahitaji. Hii inadhihirisha umuhimu wa kuwa na miundombinu ya kutosha ya elimu wakati Zanzibar ikiendelea kuendeleza maeneo ya makazi na kuvutia uwekezaji.

Shule hiyo itakuwa nguzo muhimu ya elimu ndani ya mradi mkubwa wa makazi na biashara wa Infinity Hills, unaotekelezwa na kampuni ya Infinity Developments kwa ushirikiano na Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC).

Mradi huo uliopo katika eneo la Mji Mkongwe (Stone Town) unajumuisha nyumba za makazi, maeneo ya biashara na maduka, huduma za elimu pamoja na maeneo ya burudani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Infinity Developments, Samuel Saba anasema ujenzi wa shule hiyo unaashiria uwekezaji muhimu kwa mustakabali wa Zanzibar, ukionyesha pia nia ya kampuni hiyo ya kujenga jamii zinazochangia maendeleo mapana ya kijamii na kiuchumi visiwani humo.

“Elimu ni msingi wa maendeleo ya muda mrefu ya jamii yoyote. Infinity Developments, tunaamini kuwa kujenga kwa ajili ya kesho ya Zanzibar kunamaanisha kuangalia zaidi ya nyumba na maeneo ya biashara na kuwekeza kwenye taasisi zinazosaidia familia kustawi na kuwapatia kizazi kijacho misingi ya mafanikio.

Uamuzi wa kuongeza uwezo wa Shule ya Kimataifa ya GEMS Zanzibar kutoka wanafunzi 1,100 hadi 1,500 unatokana na mahitaji yanayoongezeka na umuhimu tunaoweka katika kufanya elimu kuwa sehemu kuu ya Infinity Hills,” alisema Saba.

Aliongeza kuwa, kujumuisha elimu katika mradi uliopangwa vyema kutaweka mazingira yanayounganisha familia vizuri zaidi, huku ikisaidia ukuaji na maendeleo ya Zanzibar.

Elimu ni nguzo ya mradi wa Infinity Hills

Katika mradi wa Infinity Hills, shule hii ni sehemu ya maono mapana yanayokwenda mbali zaidi ya nyumba tu, kwa kujumuisha elimu, biashara na burudani.

Kujumuishwa kwa shule katika mazingira haya kunalenga kuongeza mvuto wa mradi huo kwa familia na kujenga jamii ambapo makazi na huduma muhimu vimepangwa pamoja.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button