Dk Mwinyi aongoza dua maalum ya Mzee Karume

KISIWANDUI, Zanzibar: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amewaongoza wananchi na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika dua maalum ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
 
Dua hiyo imefanyika leo Aprili 07, 2024, katika Ofisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Sheikh Karume aliyeuwawa Aprili 07, mwaka 1972.
 
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria dua hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Mpango, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi wengine waandamizi.