Dk. Mwinyi aongoza mamia kumzika Abbas Mwinyi

ZANZIBAR :,RAISĀ  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na mamia ya wananchi katika maziko ya kaka yake, marehemu Abbas Ali Mwinyi, aliyefariki jana.

Maziko hayo yamefanyika leo tarehe 26 Septemba 2025, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja. SOMA: Rais Samia akimfariji Dk. Mwinyi

Mapema, Dkt. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu, ndugu, jamaa na marafiki kwa Sala ya Ijumaa pamoja na Sala ya kumsalia marehemu katika Msikiti wa Jamia Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button