Dk Mwinyi apatiwa maelezo utekelezaji nishati safi

DAR ES SALAAM: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo 7 Julai, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akiwa kwenye banda hilo, alipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Neema Chalila Mbuja, ambapo alimweleza juu ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mkakati wa taifa wa nishati safi ya kupikia.

Amesema Wizara ya Nishati kupitia taasisi zilizopo chini ya wizara zimekuwa zikitekeleza kwa vitendo ajenda hiyo kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi ya kupikia kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wizara ya nishati tayari imezindua mikakati miwili ya nishati safi ya kupikia na ule wa mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo



