Dk Samia ataja mafanikio Gairo

GAIRO, Morogoro: MGOMBEA Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema katika kipindi kifupi cha miaka minne na miezi kadhaa ya uongozi wake amefanya maendeleo makubwa wilayani humo.

Akiwa kwenye kampeni ya kuinadi Ilani ya chama chake leo Agosti 30 wilayani Gairo, Morogoro, Rais Samia amenukuliwa “tumeshakamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Gairo lengo ni kuongeza fursa za vijana kujiendeleza kiujuzi pia kuongeza wigo wa ajira na kujiajiri.”

Rais Samia amesema, serikali yake imeboresha miundombinu kadhaa ya madaraja, madarasa na vituo vya afya. Hata hivyo amesema pindi akipata ridhaa tena baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba ataendelea alipoishia.

“Ninatambua bado kuna changamoto kadhaa ikiwemo ubovu wa barabara lakini tunaendelea kuzishughulikia katika kipindi changu cha pili mtakaponichagua changamoto hizo tunaenda kuzitatua.

Katika kuhitimisha hotuba yake wilayani Gairo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani humo ametoa rai kwa wananchi kushiriki haki yao ya msingi na ya kikatiba kupiga kura.

“Tarehe 29 mwezi wa 10 nendeni mkapige kura. Mkipigie kura Chama Cha Mapinduzi,” amesisitiza Rais Samia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button