Dk Samia kuwasili Manyara Oktoba 3,2025

MANYARA: Wananchi mkoani Manyara wamehimiza kujitokeza kwa wingi Oktoba 3, 2025 kumpokea mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu Hassan mkoani Manyara.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, Komrade John Nzwalile amesema mgombea urais atanadi sera na Ilani na kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani wa kata zote 142 na ubunge wa majimbo yote saba.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 30, 2025 amewaomba wananchi kufika mapema katika viwanja hivyo ili kusikiliza sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akiwa ni msemaji wa vikao halali vya chama amebainisha kuwa wilayani Hanang wamejipanga vilivyo katika mapokezi hayo kwa kukumbuka mgombea urais alipofuta machozi ya wananchi waliowengi alipokuwa Rais,kufuatia mafuriko ya maporomoko ya udongo na mawe katika Mlima Hanang na kusababisha vifo.
Ujio huo ni Sehemu ya kampeni za Udiwani, Ubunge na Rais zinazoendelea nchini ambapo wagombea wamekuwa wakipita kunadi sera za vyama vyao ambapo kwa mkoa wa Manyara mgombea urais amesema atawasili mkoani humo akitokea Arusha ambapo anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara katika kata ya Magugu wilayani Babati Vijijini na wilaya ya Hanang.
Akiwa Hanang ataongeza na wananchi katika viwanja vipya vya ‘Mount Hanang Stadium’ na kurejea Babati kwa ajili ya mapumziko.
”Siku ya tarehe 3 Oktoba 2025 ni Ijumaa mgombea urais atakuwa akitokea mkoa wa Arusha na kutarajiwa kufika Mkoa wa Manyara mchana na kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni ”
Oktoba 4, 2025 mgombea urais atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya stendi ya zamani wilayani Babati kuanzia saa tatu asubuhi kabla ya kuhitimisha ratiba yake mkoani Manyara na kuelekea Dodoma.
Kwa mujibu wa Nzwalile mkoa wa Manyara umejiandaa kwa mapokezi hayo ambayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya watu kutoka wilaya jirani za Simanjiro, Kiteto, Mbulu ikiwemo vikundi mbalimbali vya burudani na Vijana wa hamasa.
”Ni fursa adimu sana kwa Manyara, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wote kwamba tutamsikiliza mgombea urais kupitia CCM pale Magugu,Hanang na Babati. Ni mkutano wa kihistoria,” amesema Nzwalile.
”Pamoja na wakazi kutoka wilayani Babati, napata taarifa hapa kule Simanjiro wamejipanga watu zaidi ya elfu sita saba kuhudhuria,Kiteto watu zaidi ya elfu tano na kutoka Mbulu watu wengi,”amesisitiza Nzwalile.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com