WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki Februari 6, 2023.
Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Dkt. Tax ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Uturuki na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba mkubwa kwa Taifa hilo uliosabaisha vifo vya watu zaidi ya 18,000.
“Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla tunaungana na Serikali ya Uturuki katika kuombeleza msiba huo mzito,” alisema Dkt. Tax.
Mwaka 1999 Uturuki ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambapo watu wapatao 17,000 walipoteza maisha kutokana na tetemeko hilo.
Kadhalika, mwaka 2011 ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika mji wa Van lilipelekea vifo vya watu 500.