DK Tulia katika mkutano wa 27 wa maspika, wenyeviti mabunge

UGANDA: Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson,  ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 27 wa Maspika na Wenyeviti  wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika leo Januari 04, 2024 Kampala nchini Uganda.

Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.

Mkutano huu pamoja na mambo mengine unatoa fursa kwa Maspika hao kubadilishana  uzoefu wa  uendeshaji bora wa Mabunge yao.

Katika mkutano huo unaoendelea mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya jinsia na ushirikishwaji wa vijana pamoja na ujengaji wa misimamo ya pamoja ya kibunge.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button