Dk Tulia kuhutubia bunge la India

INDIA: RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson, leo Julai 19, 2024 amewasili jijini Delhi Nchini India kwa ziara ya kikazi.

Dk Tulia amepokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Bunge la India, Balozi Anjani Kumar pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega, ambapo anatarajia kutembelea Bunge la nchi hiyo na kutoa mhadhara kuhusu Demokrasia na Diplomasia ya Kibunge mapema wiki ijayo.

SOMA:https://www.instagram.com/reel/C9T6Hs3qBgA/?img_index=1

Advertisement