Dk Tulia Rais mpya Umoja wa Mabunge Duniani

ANGOLA; Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson ameshinda kwa kishindo kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uchaguzi uliofanyika leo nchini Angola.
Katika uchaguzi huo Dk Tulia amepata kura 172, wakati mpinzani wake wa karibu Catherine Gotani Hara wa Malawi alipata 61, Adji Diarra Kanouté wa Senegal alipata kura 59 na Marwa Abdibashir Hagi wa Somalia alipata kura11.
Dk Tulia anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza bunge hilo lenye nchi wanachama 179 na wabunge 705 wanaoziwakilisha nchi zao, akichukua nafasi ya Duarte Pacheco Spika wa Bunge la Ureno, ambaye alichaguliwa mwaka 2020. Pacheco amemaliza muda wake.

Habari Zifananazo

Back to top button