DAR-ES-SALAAM: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 26 Julai, 2024 ametumia usafiri wa treni ya abiria ya SGR kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro kwa ziara yake ya kikazi.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia ameipongeza Serikali kwa kuanzisha huduma hiyo ya usafiri ambayo imekuwa rafiki kwa Wananchi.
SOMA: https://www.trc.co.tz/
Sambamba na hayo, Dkt. Tulia amewataka Watanzania waendelee kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kufanya kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya siku zote kwa taifa lake.