Dodoma Sports mabingwa Kombe la Mama Samia Pamoja 

TIMU ya Dodoma Sports imeinyuka Makole Academy bao 1-0 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mama Samia Pamoja
Mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Chang’ombe yameandaliwa  na Dokii Spare Parts yakiwa na lengo la   kuhabarisha umma kupitia michezo juu ya kazi zilizofanywa na  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake katika kipindi cha miaka miwili.

Mratibu wa mashindano hayo Ummy  Wenceslaus ‘Dokii’  amesema mashindano hayo yatafanyika nchi nzima.

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amezipongeza timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo na kutumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya michezo ambapo kwa Dodoma Jiji mradi wa ujenzi wa Sports Arena unaanza kutekelezwa na itakuwa fursa kubwa kwa vijana wa Dodoma kutumia miundombinu hiyo kujiendeleza katika vipaji vyao.
Mashindano hayo pia yalihudhuriwa na Bondia maarufu nchini Karimu Mandonga na Mtangazaji wa EFM Oscar Oscar
Advertisement
/* */