Dortmund mwamba unaotamba pande zote

PARIS, Ufaransa: USIKU wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UCL) umeendelea kwa hatua ya mkondo wa pili wa Nusu Fainali, rekodi kadhaa zimewekwa, kuvunjwa na wababe wa Ujerumani, Borussia Dortmund kufuatia kuwafungashia virago mabingwa wa Ligue 1 ya Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG) kwa kipigo cha 0-2 mbele ya mashabiki wao 46,435 waliojazana katika dimba la Parc des Princes.
Ushindi wa hapo jana unaturejesha miaka 11 nyuma hadi msimu wa UCL mwaka 2013 walipotinga fainali ya UCL kwa kuiondosha Real Madrid kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Safu ya ulinzi ya Dortmund imeonesha ubora wa pekee kwa kuizuia PSG kufunga goli lolote katika michezo yote miwili ya nusu fainali.
Rekodi chafu kwa PSG, mosi kwa kurekodi idadi kubwa zaidi ya mashuti katika mchezo wa mtoano wa UCL bila ya kufunga tangu kuanza kutunzwa kwa kumbukumbu hizo msimu wa mwaka 2003-04.
PSG imepiga mashuti 30 huku matano yakilenga lango bila kufunga goli, manne yakigonga mwamba wa goli.
Goli la Uamuzi la Mats Hummels dakika ya 50 ya kipindi cha pili cha mchezo huo wa mkondo wa pili, ambalo liliipa Dortmund uongozi ambao waliudumisha kwa muda uliobaki wa mchezo, Hummels na Marco Reus ndio wachezaji pekee waliyoshuhudia kikosi hicho kikitinga fainali UCL miaka 11 iliyopita.
Matukio haya bila shaka yameacha alama katika historia ya mashindano hayo na yamekuwa ya kukumbukwa kwa mashabiki wa pande zote mbili kwa sababu tofauti.
Mafanikio ya Dortmund ni ya kipekee hasa wanapojiandaa kwa fainali itakayofanyika Wembley, huku PSG wakitafakari juu ya nafasi hii waliyopoteza.
Rejea: https://habarileo.co.tz/timu-zilizofuzu-16-bora-uefa/



