Dozi za malaria milioni kumi zatolewa Afrika

GENEVA: Ushirikiano wa Kimataifa wa Chanjo- Gavi umesema karibu dozi milioni 10 za Malaria zilipelekwa barani Afrika katika mwaka wa kwanza wa utoaji wa kawaida wa chanjo kote barani humo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo umeonyesha kuwa zaidi ya dozi milioni 9.8 zimetolewa na angalau watoto milioni tano wamepata ulinzi wa kutosha. SOMA: WHO yatangaza hakuna malaria Misri
Kulingana na Gavi, programu hiyo inalenga kutoa chanjo nne kwa kila mtoto na kusisitiza kwamba kila mara ulilenga kuwafikia watu wanaokabiliwa na kitisho zaidi katika kila nchi.
Shirika la Afya Duniani- WHO limesema ugonjwa wa Malaria huua karibu watu 600,000 kwa mwaka, wengi zaidi kutoka Afrika, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.



