MISRI : MKUU wa Shirika la Afya Duniani – WHO, Tedros Adhanom ametangaza ugonjwa wa malaria Misri utabaki kuwa historia .
“Malaria ni ugonjwa wa zamani lakini ugonjwa huu uliwasumbua wengi nchini humo lakini sasa ni historia,” alisema Tedros.
Katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini humo, Misri iliamua kuchukua hatua za kutokomeza ugonjwa huo ambao unaoenezwa kwa njia ya mbu kwa asilimia 100.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani ugonjwa wa malaria huua watu wasiopungua 600,000 kila mwaka na karibu wote kutoka barani Afrika.