CONGO: SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imezindua rasmi kampeni yake ya kuwania kiti kisicho cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha 2026-2027.
Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Therese Kayikwamba Wagner, amesema kuwa ikiwa taifa hilo litachaguliwa, litakuwa na jukumu la kushawishi dunia kufanya mageuzi ya kujenga amani katika ngazi za kimataifa. SOMA:Hatma DR Congo Rwanda haijulikani
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaundwa na wanachama watano wa kudumu ambao ni China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani pamoja na wanachama 10 wasio wa kudumu, ambao wanachaguliwa kwa mihula ya miaka miwili.
DRC imewahi kuchaguliwa mara mbili kuwa mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama, mwaka 1982 hadi 1983 na mwaka 1991 hadi 1992 wakati wa Vita vya Ghuba.