DR Congo yakanusha kukamatwa FDLR

DR CONGO : JESHI la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limetangaza kukataa taarifa za kukamatwa kwa wapiganaji 20 wa kundi linalohusishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, katika ardhi yake.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kundi la M23, linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, kutangaza kuwa limewakamata wapiganaji wa kundi la FDLR, ambalo linaundwa na jamii ya Wahutu na linaaminika kuhusika na mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Jeshi la Congo limekanusha vikali madai hayo na kusema kuwa ni ya uongo, huku likidai kuwa hata video iliyoonesha wapiganaji wakikabidhiwa kwa Rwanda ni taarifa za uongo.

Kwa muda mrefu, Rwanda imekuwa ikidai kuwa kundi la FDLR linahusika na machafuko katika eneo la Mashariki mwa Congo, na imekuwa ikitumia madai hayo kama msingi wa kuhalalisha uungaji mkono kwa kundi la M23.

Soma: Watu 7,000 wafa DR Congo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button