KOREA KUSINI : Korea Kusini kupiga kura ya kumuondoa madarakani Makamu wa Rais, Han Duck-soo, wiki mbili baada ya bunge kupiga kura ya kumshtaki Rais Yoon Suk Yeol.
Baadhi ya wabunge 192 walipiga kura ya kumuondoa madarakani ambapo kura zinazohitajika ni 151. SOMA: Rais Yoon hatarini kuondolewa madarakani Korea Kusini
Waziri Mkuu Han alichukua wadhifa huo baada ya Rais Yoon kuondolewa madarakani na bunge kufuatia jaribio lake lisilofanikiwalililogonga mwamba la kuweka sheria ya kijeshi tarehe 3 Disemba.
Han alitakiwa kuiongoza nchi hiyo kutoka katika msukosuko wa kisiasa, lakini wabunge wa upinzani walidai kuwa alikuwa akikataa matakwa ya kukamilisha mchakato wa kumuondoa Yoon.