Ebola yaibuka tena Congo

DR CONGO : SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema mripuko wa Ebola ulioanza mwanzoni mwa Septemba nchini DRC umesababisha vifo vya watu 42, huku wengine 64 wakithibitishwa kuambukizwa na ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema shirika lake pamoja na washirika wake wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya DRC kudhibiti ugonjwa huo. Wizara ya afya nchini humo ilianza kutoa chanjo wiki mbili zilizopita.
Ebola, ugonjwa unaoambukizwa kupitia majimaji ya mwili, umesababisha vifo vya takriban 15,000 barani Afrika katika miongo mitano iliyopita. Mripuko mkubwa wa Ebola uliotokea DRC kati ya 2018 na 2020 uliua takriban watu 2,300. SOMA: Wahudumu afya wapatiwa chanjo kudhibiti Ebola



