SIERRA LEONE : WAZIRI wa Afya nchini Sierra Leone, Austin Demby amesema serikali imezindua kampeni ya chanjo ya kitaifa dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa wafanyakazi wa afya baada ya mlipuko wa ugonjwa kutokea katika nchi hiyo.
Demby amesema chanjo hizo zitawafikia wahudumu wa afya 20,000 ambao watapatiwa chanjo hiyo.
Aidha amesema wahudumu wa afya ni kundi ambalo linakabiliwa na hatari ya maambukizi kabla ya kuwafikia wagonjwa kadhalika na madereva wanaobeba wagonjwa wa Ebola.
Kundi lingine ambalo litapatiwa chanjo ni kundi la waganga wa kienyeji na washauri ambao mara nyingi wa kwanza kuwasiliana na wagonjwa.
Demby ameongezea kuwa utoaji wa chanjo hiyo ya Ebola utaweza kulinda vyema mfumo wa huduma ya afya na wafanyakazi wake dhidi ya ugonjwa huo ili kupunguza madhara ndani ya jamii. SOMA : Virusi vya Ebola hukaa kwenye mbegu za kiume