Virusi vya Ebola hukaa kwenye mbegu za kiume

MWANAUME akipata ugonjwa wa Ebola na akafanikiwa kupona, anapaswa kukaa miezi sita bila kujamiiana kwa kuwa virusi vya ugonjwa huo uendelea kuishi kwenye mbegu za kiume kwa kipindi hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Kinga na Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko kutoka Wizara ya Afya, Dk Joseph Hokororo amesema kirusi hicho kinaweza kuishi kwenye maeneo ya maji maji kwa muda wa miezi sita, na eneo kavu kinaweza kuishi kwa saa kadhaa.

Amesema mbali na kwenye mbegu za kiume pia kirusi hicho kinauwezo wa kukaa kwenye Kondo la Nyuma la Mama (Placenta).

Advertisement

Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.

Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa.

Akizungumza anasema “Ugonjwa wa Ebola uua kwa asilimia 40, hii maana yake ni kuwa kati ya watu 100 waliogua Watu 40 mpaka 90 wanapoteza maisha.”Amesema na kuongeza

“Iwapo mwanaume akabahatika kupona basi anapaswa kukaa miezi sita bila kukutana na mwanamke kwa kuwa licha  ya kupona kirusi hicho kitaendelea kuishi kwenye mbegu zake za kiume kwa miezi sita hivyo akikutana kimwili na mwanamke atamuambukiza Ebola.”Amesema Hokororo

Aidha, amesema ugonjwa huo wa Ebola umetokana na kirusi kilichotoka  kwa Nyani, Popo na Sokwe kwenda kwa binadamu ambapo ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ya maji maji kama jasho la mwili, mate, matapishi na majimaji mengine.

Pia kirusi hicho kinauwezo wa kukaa maeneo makavu kama kwenye mlango, koki za bomba, meza na maeneo mengine hivyo kushauri watu kunawa mikono na maji tiririka na sabuni mara kwa mara ili kujikinga na ugonjwa huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *