ECOWAS yatangaza muundo mpya wa majadilino kwa nchi zilizojiondoa.

NIGERIA : MAKAO MAKUU ya kiutawala ya Kamisheni ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) yameanzisha muundo mpya wa kuwezesha majadiliano na nchi tatu zinazojiondoa rasmi kutoka kwenye jumuiya, ikiwemo Burkina Faso, Mali, na Niger, ambapo mchakato huo utaanza rasmi leo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano asubuhi, Tume ya ECOWAS imesema kuwa inakusudia kupunguza mkanganyiko na usumbufu kwa wananchi na biashara zinazohusiana na ECOWAS na zile za nchi za Sahel wakati wa kipindi cha mpito.

“Kujiondoa kwa Burkina Faso, Mali na Niger kutoka ECOWAS kumeanza kutekelezwa rasmi tarehe 29 Januari 2025,” ilisema taarifa hiyo. SOMA: NIGERIA: Hatma ya Burkina Faso, Mali na Niger kujulikana kesho

Hata hivyo, ili kudumisha mshikamano wa S kikanda, ECOWAS imeomba mamlaka zote ndani na nje ya Nchi Wanachama kuwaruhusu raia wa nchi hizo tatu kuendelea kufurahia haki ya usafiri bila visa, kufanya biashara bila kuingiliwa, na kuishi kwa mujibu wa itifaki za ECOWAS hadi itakapotolewa tangazo lingine.

Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwa ECOWAS itaendelea kutambua hati za kusafiria na vitambulisho vyenye nembo ya ECOWAS kwa raia wa Burkina Faso, Mali, na Niger.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button