Elimu yahitajika kunufaika na teknolojia

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa, Lawrence Mafuru amesema ili nchi iweze kunufaika na teknolojia pamoja na mabadiliko ya mapinduzi ya viwanda ni lazima watu wapate elimu.

Mafuru amesema hayo katika kongamano la 27 la mwaka lililojadili masuala ya utafiti mkoani Dar es Salaam, na kuandaliwa na Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umaskini Tanzania (Repoa).

Akifafanua hilo, Mafuru amesema elimu hiyo sio tu ile ya kufaulu mitihani bali inayowapa stadi na kufanya shughuli za kiuchumi.

“Uwekezaji katika maeneo hayo utasaidia kukuza uchumi na kuondoa umaskini,” amesema.

Pia amesema nchini Tanzania eneo kubwa ambalo linaangaliwa kuleta mabadiliko ya haraka ni kuboresha sekta ya kilimo na kuifanya iwe na uzalishaji wenye tija.

“Kwanza itakuwa na manufaa mengi kwa sababu sasa soko la mazao ya kilimo ni kubwa sio tu hapa nchini lakini kwa nchi zinazotuzunguka,” amesema.

Ameshauri nchi kuendelea kuwa na utayari na mabadiliko ya tabia nchi hasa katika sekta ya kilimo na hata kwenye maisha ya kawaida.

“Unataka uendelea kuwa shughuli za uchumi zisizosimama kwa sababu ya mafuriko, na mafuriko yanatokana na ujenzi, uharibifu wa mazingira kwa hiyo tunapopanga mipango ya maendeleo tukumbuke pia kutunza mazingira ili mipango yetu isiharibiwe na shughuli hizo zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Repoa, Profesa Rwekaza Mukandala amesema ni wakati muafaka wa kuangalia kiini cha uchumi katika muda huu ambao taifa lipo kwenye matayarisho ya mpango mkakati mpya wa miaka 50.

“Kwa mfano watanzania wengi asilimia 70 wapo katika kilimo lakini uzalishaji ni duni, teknolojia inayotumika ni ya zamani, mapato yanayopatikana ni madogo.

“Kuna haja ya kuangalia njia ambazo tunaweza tukaleta mabadiliko katika uchumi, katika ufugaji, uvuvi kuhakikisha tunatumia teknolojia za juu zaidi, tunatumia mbinu mpya zaidi na tunatumia uchumi wa kidijitali, mawasiliano makubwa zaidi, tunauza nje zaidi na tunauza vitu vilivyochakatwa tayari ili kuongeza thamani ya hayo tunayoyauza,” amesema.

Amesema kuna haja ya kujipanga upya kwa kuwa kuendelea kutumia njia zile zile za kizamani, kuzalisha kwa teknolojia zile zile za kizamani hata ikija miaka 50 zaidi taifa litakuwa lipo pale pale.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dk Donald Mmari amesema moja ya tatizo ambalo linafanya ukuaji wa uchumi usiwe na matokeo mazuri katika kujenga ajira na kupunguza umaskini ni muundo wa uchumi.

Amesema kupitia kongamano hilo wataalamu, watafiti na watunga sera wataangalia ni kwa namna gani wanaweza kubadilisha muundo wa uchumi ili ukue kwa kasi lakini uweze kuwa jumuishi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
namongo FC
namongo FC
23 days ago

WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)..

336385342_23852687669090184_4327056666681808736_n.jpeg
MeghanFoster
MeghanFoster
Reply to  namongo FC
22 days ago

I get paid more than $120 to $130 every hour for working on the web. I found out about this activity 3 months prior and subsequent to joining this I have earned effectively $15k from this without having internet working abilities copy underneath site to check it.
.
.
Detail Here—————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

namongo FC
namongo FC
23 days ago

WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI).

396913935_270519422649565_3279129179102033513_n-1699514567.7649-232x300.jpg
namongo FC
namongo FC
23 days ago

WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)….

400652614_122123967464061853_6811123058608430011_n-1699514588.5978-200x300.jpg
namongo FC
namongo FC
23 days ago

WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)../

400691249_864990868631687_149643332150728266_n-1699514610.2614.jpg
babofe8659
23 days ago

 JOIN US I’m making a good salary from home 16580-47065/ Doller week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………> http://profitguru7.com

namongo FC
namongo FC
23 days ago

USALAMA KAZI MHE TUTAFANYA KWA AJILI YA “MLIMA KILIMAJARO” – LAZIMA TUFANYE KITU KWA AJILI YA TANZANIA USALAMA WETU TUKITEMBELE

OSK.jpeg
MarieAllen
MarieAllen
23 days ago

Everybody can earn 500 dollars Daily…(Qg) Yes! you can earn more than you think by working online from home. I have been doing this job for like a few weeks and my last week payment was exactly 25370 dollars. 
.
.
.
COPY This Website OPEN HERE……….> > > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x