DAR-ES-SALAAM, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko amesema asilimia kubwa ya Watanzania bado hawana ufahamu wa kutosha kuhusu Uchumi wa Buluu .
Akihutubia wadau wa sekta ya bahari katika Kongamano la tatu la Kimataifa la Uchumi wa Buluu linalofanyika jijijini Dar es Salaam, Dk Biteko amesema tafsiri kamili ya Uchumi wa Buluu bado haijaweza kufahamika kwa wengi wakiwemo Watanzania na viongozi.
Isome:https://habarileo.co.tz/dk-biteko-afungua-kongamano-uchumi-wa-buluu/
Amesema jitihada inayohitajika kwa sasa ni kuelimisha umma kuhusu fursa na rasilimali za bahari zinazopatikana, ili watu wengi wawe na ufahamu kwa maslahi ya taifa.
“Kwa hiyo utaona mawanda ya kujadili uchumi wa buluu bado ni changamoto si tu kwa wananchi hata sisi tunaosimamia sekta mbalimbali,” amesema Dk Biteko.