Mwongozo mpya BMUs kulinda rasilimali za uvuvi

DODOM: WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Dk Bashiru Ally amezindua Mwongozo wa Kitaifa wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Nchini (BMUs) ili kulinda rasilimali hizo ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi na kuimarisha usalama wa chakula.

Dk Bashiru alizindua mwongozo huo jana Machi 25, 2026 wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa ngazi ya juu kuhusu mustakabali wa uendelevu na usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi na uchumi wa buluu aliofanyika Jijini Dodoma.

Aidha, alitoa rai kwa wataalam, viongozi na wadau wa sekta ya uvuvi nchini kutafuta mbinu shirikishi katika kukabiliana na uvuvi usiofuata sheria.

“Nimefanya ziara Kanda ya Ziwa nimeona kuna watu wanafanya ubunifu wa uhalifu kwa kubadilisha nyavu halali kufanya uvuvi usiofuata sheria, utaratibu wa namna ile huwezi kudhibiti kwa polisi, utakuwa na polisi wangapi ?, njia pekee ya kufanikiwa ni kuwa na mbinu shirikishi na kuelimishana bila kuchoka, kwa hiyo huu mwongozo usiishie kwenye makaratasi” alisema Dk Bashiru.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (TNC), Lucy Magembe alisema shirika hilo na Wizara ya mifugo na uvuvi hufanya ushirikishwaji wa wavuvi katika uhifadhi na kusimamia rasilimali za uvuvi, kupitia Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Nchini (BMUs) katika kuimarisha uvuvi endelevu na uchumi wa buluu nchini.

“Tumekuwa tukitoa sayansi na elimu ya uvuvi bora, kushirikiana na wananchi kupunguza uvuvi haramu ili kudumisha uvuvi endelevu” alisema Magembe.

Awali Naibu Katibu Mkuu anayesimamia sekta ya uvuvi Profesa Mohamed Sheikh alisema ulinzi wa rasilimali uvuvi ni jukumu la kila mtu na kwamba vikundi takriban 700 vya BMUs nchini vimekuwa vikishirikiana na wananchi katika kusimamia na kulinda rasilimali za uvuvi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button