‘Elite’, matumizi ya kadi yaipaisha Exim

Dar es Salaam: Uongozi wa Mastercard leo umeitembelea ofisi za Benki ya Exim jijini Dar es Salaam leo na kuikabidhi taasisi hiyo ya fedha tuzo mbili kutokana na ufanisi wake.
kukabidhi tuzo mbili muhimu kutokana na mafanikio ya Benki hiyo kwa mwaka 2025.umefanya meitembelea eo imefanya ziara yake maalumu katika makao makuu ya , kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo na
Katika ziara hiyo, Benki ya Exim ilitunukiwa tuzo ya “Best Elite Banking Proposition – 2025” pamoja na tuzo ya “Highest Spend Per Card in Tanzania – 2025”, zikionesha mafanikio yake katika kubuni na kuendesha huduma za kibenki za hadhi ya juu pamoja na kuongoza kwa matumizi ya kadi nchini Tanzania.
Tuzo hizi zinatokana na mafanikio yaliyopatikana kufuatia uzinduzi wa huduma ya Elite Banking mnamo Julai 2025, huduma iliyolenga kuwahudumia wateja wa hadhi ya juu (High-Net-Worth Individuals) kwa suluhisho za kifedha zilizobuniwa mahsusi kulingana na mahitaji yao kulingana na mfumo wao wa maisha. Kupitia huduma hii, wateja wanapatiwa Meneja Mahusiano binafsi, anayetoa suluhisho za uwekezaji na mikopo kwa ajili ya mtu binafsi, pamoja na kufaidika na ofa ya kimataifa ikiwemo upatikanaji wa lounge za viwanja vya ndege kupitia Mastercard DragonPass.
SOMA: Exim yaboresha utoaji mikopo kwa watumishi wa umma kupitia Utumishi Portal
Aidha, tuzo ya “Highest Spend Per Card” inaonesha mafanikio ya Benki katika kuhamasisha matumizi ya kadi kwa wateja wake, hatua iliyochangiwa na kampeni mbalimbali za kimkakati ikiwemo UEFA Priceless Campaign, ambayo ilihamasisha malipo kwa kutumia kadi huku ikitoa fursa za kipekee za kufurahia ofa za kimataifa kwa washindi wake.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew Lyimo, alisema: “Tuzo hizi kutoka Mastercard ni uthibitisho wa mkakati wetu wa kubadilisha na kuinua viwango vya huduma za kibenki za hadhi ya juu nchini Tanzania.
“Uzinduzi wa Elite Banking mwaka 2025 ulikuwa hatua muhimu katika safari yetu ya kuwahudumia wateja wetu kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuunganisha suluhisho za kifedha zilizo bora na ofa za kipekee kulingana na mfumo wa maisha ya wateja wetu. Mafanikio haya yanatokana na imani ya wateja wetu pamoja na uwekezaji wetu endelevu katika ubunifu na teknolojia.”
Naye Makamu Rais na Meneja wa akaunti wa Master Card, Elsie Kaguru alisema kuwa Benki ya Exim imeonesha uongozi wa kipekee katika kukuza huduma za “premium Banking” na kuimarisha matumizi ya kadi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Kaguru, ukuaji wa haraka wa huduma ya “Elite Banking” pamoja na kiwango cha juu cha matumizi kwa kila kadi vinaakisi uelewa sahihi wa mahitaji ya wateja wa kisasa.
“Tunajivunia ushirikiano wetu na Benki ya Exim na tuna matarajio makubwa ya kuendeleza mafanikio haya kwa pamoja,” alisema.
Ushirikiano kati ya Exim Bank na Mastercard umejikita katika kuimarisha mifumo salama ya malipo ya kidijitali, kuboresha huduma za kadi za hadhi ya juu, na kupanua upatikanaji wa manufaa ya kimataifa kwa wateja wa Tanzania. Ushirikiano huu umeleta matokeo yanayoonekana katika utofautishaji wa bidhaa pamoja na ongezeko la utendaji wa miamala.



